Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi atembelea Maonyesho ya Nane Nane Morogoro - Issa Michuzi | PressTZ - Your Number 1 Source of Aggregated Online Content

 

Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi atembelea Maonyesho ya Nane Nane Morogoro

Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi amesema umefika sasa kwa kwa Wizara na Taasisi zinazohusika na Sekta ya Elimu Nchini kumuandaa Mwanafunzi katika masomo ya Kilimo kuanzia ngazi ya Msingi hadi Sekondari ili atakapofikia uwezo wa kuingia chuo Kikuu awe tayari ameshaelewa nini Kilimo.Alisema uingizwaji wa  Mitaala ya Kilimo ndani ya masomo ya kawaida maskulini itamuwezesha Wanafunzi kujitayarisha mapema katika muelekeo wa kujijengea uwezo wa ajira ya uhakika ndani ya Sekta ya Kilimo wakati amalizapo masomo yake ili aweze kujitegemea kupitia Sekta hiyo muhimu kwa uchumi wa Taifa.Balozi Seif Ali Iddi alitoa ushauri wakati akizungumza na vyombo mbali mbali vya Habari mara  baada ya kumaliza ziara yake ya kuangalia Maonyesho  mbali mbali ya Siku ya Nane Nane yanayofanyika katika Viwanja vya Mwalimu Julius Kambarage Nyerere Mkoani Morogoro. Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi akivishwa Skafu na Vijana Chipukizi wa Morogoro mara alipoingia kwenye U... Continue reading ->


Source: Issa MichuziRead More