MAKAMU WA RAIS AENDELEA NA ZIARA WILAYANI ROMBO - Issa Michuzi | PressTZ - Your Number 1 Source of Aggregated Online Content

 

MAKAMU WA RAIS AENDELEA NA ZIARA WILAYANI ROMBO
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan amewataka Watumishi wa Serikali Wilayani Rombo kufanya kazi kwa kushirikiana.
Makamu wa Rais ameyasema hayo jana  mara baada ya kupokea taarifa ya Wilaya hiyo kutoka kwa Mkuu wa Wilaya Mhe. Agnes Hokororo.
“Wote tunajenga nyumba inayoitwa Tanzania katika nafasi yako yoyote ulipo unajenga nyumba inayitwa Tanzania, kwa itikadi yako yoyote uliyonayo unajenga nyumba inayoitwa Tanzania tunatawaliwa na sheria moja, tunataliwa na miongozo hiyo hiyo ya Serikali, kanuni na mambo mengine na hiyo hiyo Serikali”.
Katika ziara yake Wilayani Rombo Makamu wa Rais alikagua maendeleo ya mradi wa ujenzi wa Jengo la Utawala la Halmashauri ya Rombo, mradi wa maji Shimbi Mashariki,kukagua shamba la Miti Rongai.
Makamu wa Rais ambaye yupo kwenye ziara ya kukagua na kuhamasisha shughuli za maendeleo pia alipata nafasi ya kuwasalimu wananchi wa Tarakea waliojitokeza barabarani kumsalimia na alih... Continue reading ->Source: Issa MichuziRead More