MAKAMU WA RAIS AKUTANA NA KUZUNGUMZA NA MKURUGENZI WA UN WOMAN - Issa Michuzi | PressTZ - Your Number 1 Source of Aggregated Online Content

 

MAKAMU WA RAIS AKUTANA NA KUZUNGUMZA NA MKURUGENZI WA UN WOMAN

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan, amelitaka Shirika la Umoja wa Mataifa linaloshuhulikia Wanawake Duniani  (UN WOMAN)  kuandaa Tathmini ya kinchi kuhusiana na Kongamano la Beijing.
Amesema ni Vyema kuwepo na uwezekano wa kuweza kuandaa Tathmini ya uhakika itakayoweza kuonesha hali halisi ya Idadi ya Wanawake waliopo katika Nafasi mbalimbali za Kiuongozi hususan kwenye Baadhi ya Mashirika na Taasisi Binafsi.
Makamu wa Rais ameyasema hayo leo Agost 14, 2019 Ofisini kwake Ikulu Jijini Dar Es Salaam wakati alipokutana na kuzungumza na Mkurugenzi Mkazi wa Shirika la Umoja wa Mataifa linaloshuhulikia Wanawake Duniani (UN WOMAN) Bibi Hodan Addou.
 Aidha Makamu wa Rais amelishukuru Shirika la Umoja wa Mataifa linaloshuhulikia Wanawake Duniani  (UN WOMAN) kwa kuendelea kuweza kutoa fursa katika nyanja mbalimbali za Kijamii na kimaendeleo kwa Wanawake Duniani na kulitaka Shirika hilo kuendelea kuzidi kutoa fursa hizo kwa Wanawake Hususan kwenye sekta za... Continue reading ->


Source: Issa MichuziRead More