MAKAMU WA RAIS AKUTANA NA UJUMBE WA TAASISI YA MAENDELEO YA ODI KUTOKA NCHINI UINGEREZA - Issa Michuzi | PressTZ - Your Number 1 Source of Aggregated Online Content

 

MAKAMU WA RAIS AKUTANA NA UJUMBE WA TAASISI YA MAENDELEO YA ODI KUTOKA NCHINI UINGEREZA

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan leo amekutana na Mkuu wa Utafiti na Mkurugenzi wa Mpango wa kusaidia Mabadiliko ya Kiuchumi kutoka Taasisi ya Maendeleo ya Kimataifa (ODI) kutoka nchini Uingereza Dkt. Dirk Willem te Verde na ujumbe wake, Ikulu jijini Dar es Salaam.Makamu wa Rais amesema Ujumbe huo unataka kutoa ushirikiano katika mpango wetu wa uchumi wa viwanda Tanzania.Katika mkutano huo ambao pia ulihudhuriwa na Waziri wa Fedha na Mipango Dkt. Philip Mpango pamoja na Viongozi na Wataalam wa masuala ya Viwanda na Uchumi nchini.Nae, Waziri wa Fedha na Mipango Dkt. Philip Mpango amesema kuwa Taasisi hiyo imekuja kufanya mazungumzo na Serikali ili kuharakisha utekelezaji wa Mpango wa Kiuchumi.Kwa upande wake Mkuu wa Utafiti kutoka Taasisi hiyo Dkt. Dirk Willem te Verde ameahidi kutoa ushirikiano wa kutosha kwa Serikali ya Tanzania katika kufanikisha mpango wa kuwa na Tanzania ya Viwanda.
 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Sa... Continue reading ->


Source: Issa MichuziRead More