MAKAMU WA RAIS AMALIZA ZIARA MKOANI MANYARA NA KUREJEA DODOMA - Issa Michuzi | PressTZ - Your Number 1 Source of Aggregated Online Content

 

MAKAMU WA RAIS AMALIZA ZIARA MKOANI MANYARA NA KUREJEA DODOMA

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan leo amemaliza ziara yake ya siku 5 mkoani Manyara. Akizungumza kwenye kikao cha majumuisho ambacho kilihudhuriwa na Viongozi na Watendaji wa mkoa huo Makamu wa Rais aliwapongeza kwa kazi nzuri wanayofanya na kuainisha maeneo kadhaa ambayo yanatakiwa kutupiwa jicho.
Baadhi ya maeneo hayo ni Mazingira ambapo aliuambia Uongozi huo kupanda miti ya kutosha, kulinda maeneo yanayochimbwa madini kuwa kuwasimamia wachimbaji katika kutunza mazingira pamoja na kutunza vyanzo vya maji. Eneo jingine alilozungumzia Makamu wa Rais ni suala zima la Lishe bora kwa watoto na kuhamasisha wananchi kuwa na Bima ya Afya.
Makamu wa Rais ameutaka Uongozi wa mkoa huo kuliangalia suala la mimba za utotoni ambalo kwa kiasi kikubwa linaupa mkoa sura mbaya ambapo mpaka sasa kwa mujibu wa ripoti zaidi ya watoto 4200 wamepata mimba wakiwa na umri mdogo.
“Njia pekee ya kuwalinda watoto wa Kike ni kuwapeleka shule”alisema Makamu wa Rais. Ai... Continue reading ->


Source: Issa MichuziRead More