MAKAMU WA RAIS AONGOZA KONGAMANO LA KUMPONGEZA RAIS SHEIN - Issa Michuzi | PressTZ - Your Number 1 Source of Aggregated Online Content

 

MAKAMU WA RAIS AONGOZA KONGAMANO LA KUMPONGEZA RAIS SHEIN

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan ametoa wito kwa Umoja wa Wanawake Tanzania (UWT) na wanawake kwa ujumla kuchapa kazi zaidi na kushikamana katika kuleta maendeleo kwa jamii nzima.
Makamu wa Rais ameyasema hayo kwenye Kongamano la Wanawake la Kumpongeza Mheshimiwa Dkt. Ali Mohammed Shein, Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi  kwa kutekeleza ilani ya Uchaguzi ya Chama cha Mapinduzi lililofanyika kwenye hoteli ya Verde, wilaya ya Magharibi A, mkoa wa Mjini Magharibi, Unguja.
“Sisi ni sehemu muhimu sana ya utekelezaji wa ilani ya uchaguzi ya Chama Cha Mapinduzi, hivyo Kongamano hili liwe chachu yetu katika kuchapa kazi zaidi”alisema Makamu wa Rais.
Aidha, aliwasihi wanawake kuchukua jukumu la kuzisemea na kuzitangaza kwa sauti kubwa kazi nzuri zinazofanywa na viongozi  wa Serikali zetu mbili ili wananchi wazijue na wasipotoshwe.
“Sote ni mashuhuda wa kazi kubwa na nzuri iliyofanyika hapa Zanzibar kwa kipindi cha miaka mitatu. S... Continue reading ->


Source: Issa MichuziRead More