MAKAMU WA RAIS AZINDUA BARABARA MPYA YA BONITE MANISPAA YA MOSHI - Issa Michuzi | PressTZ - Your Number 1 Source of Aggregated Online Content

 

MAKAMU WA RAIS AZINDUA BARABARA MPYA YA BONITE MANISPAA YA MOSHI

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan amesema Serikali ya Awamu ya Tano imedhamiria kupeleka huduma bora za kimaendeleo kwa wananchi wote nchini.
Makamu wa Rais ameyasema hayo leo wakati wa uzinduzi wa barabara iliyojengwa kwa kiwango cha lami ya Bonite yenye urefu wa kilometa 2.93 iliyopo katika Manispaa ya Moshi. 
Makamu wa Rais yupo mkoani Kilimanjaro kwenye ziara ya kukagua na kuhamasisha shughuli za maendeleo.“Nawapongeza kwa Usafi na nawapongeza kwa miundombinu ya ndani katika Manispaa ya Moshi, Serikali yetu inaleta maendeleo kwa kila Mtanzania” alisema Makamu wa Rais.
Makamu wa Rais anaendelea na ziara yake ya kukagua na kuhamasisha shughuli za maendeleo mkoani Kilimanjaro ambapo pamoja na kufungua barabara ya Bonite pia aliweka jiwe la msingi la mradi wa ujenzi wa Kituo cha Afya Pasua ambacho kimegharimu shilingi za Kitanzania milioni 400 na kitakuwa na Wodi ya Mama na Mtoto, Chumba cha Upasuaji, Xray na Maabara.
Kwa Upande wake Waziri wa ... Continue reading ->


Source: Issa MichuziRead More