MAKAMU WA RAIS AZINDUA JENGO GHOROFA MBILI LA KITUO CHA MAMA NA MTOTO KMKM KIBWENI ZANZIBAR - Issa Michuzi | PressTZ - Your Number 1 Source of Aggregated Online Content

 

MAKAMU WA RAIS AZINDUA JENGO GHOROFA MBILI LA KITUO CHA MAMA NA MTOTO KMKM KIBWENI ZANZIBAR

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan amewataka wanaotoa huduma katika sekta ya afya kutoa Huduma bora.Makamu wa Rais ameyasema hayo leo wakati wa uzinduzi wa jengo la kituo cha Mama na Mtoto katika hospitali ya KMKM Kibweni ikiwa sehemu ya maadhimisho ya shamrashamra za kutimiza miaka 55 ya Mapinduzi ya Zanzibar.
Makamu wa Rais ametoa rai kwa Wataalamu wa Afya nchini kutambua kuwa wanatakiwa kutumia utaalamu wao katika kuokoa maisha ya mama na mtoto ili kuepuka vifo vitokanavyo na uzazi kwa ajili ya kujenga Taifa lenye kizazi imara. “Ni wajibu wenu kutumia utaalamu wenu na jukumu mlilopewa na Taifa katika kuleta mabadiliko ya kiutendaji na ufanisi katika sekta ya afya nchini” alisema Makamu wa Rais.
Jengo la Kituo cha Mama na Mtoto ni la ghorofa mbili na limegharimu jumla ya shilingi 3, 648,400,000/- na kuzingatia watu wenye mahitaji maalumu.
Huduma zitakazopatikana kwenye jengo hilo la ghorofa mbili ni Huduma ya Mama na Mtoto, Wodi ya Wazazi na Watoto... Continue reading ->


Source: Issa MichuziRead More