MAKAMU WA RAIS AZINDUA URITHI FESTIVAL - Issa Michuzi | PressTZ - Your Number 1 Source of Aggregated Online Content

 

MAKAMU WA RAIS AZINDUA URITHI FESTIVAL

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan amesema kwa kutambua umuhimu wa sekta ya utalii kwa uchumi wa nchi yetu, na kwamba ili kuweza kupata watalii wengi zaidi lazima kuwa na usafiri wa anga ulio na uhakika; ndiyo maana Serikali imeamua kufufua shirika letu la ndege (ATCL) na tayari Serikali imenunua ndege mpya saba.
Makamu wa Rais ameyasema hayo leo wakati wa sherehe za uzinduzi wa Tamasha la Mwezi  wa Urithi wa Utamaduni wa Mtanzania linalojulikana kama Urithi Festival liliofanyika kwenye uwanja wa Jamhuri, Jijini Dodoma.
“Ni wazi pia kwamba utalii unahitaji usafiri bora na wa uhakika wa nchi kavu, hususan reli na barabara.  Kwa kujua hili, Serikali imeamua kujenga reli mpya ya Standard Gauge kutoka Dar es Salaam hadi Dodoma, katika awamu hii ya kwanza. Vilevile, Serikali inakarabati reli yetu ya zamani kutoka Tanga hadi Arusha. Ukarabati wa reli hii utawezesha pia kuanzisha utalii wa reli (railway tourism) utakaohusisha vivutio mbalimbali, husus... Continue reading ->


Source: Issa MichuziRead More