MAKAMU WA RAIS AZINDUA USHIRIKA WA MAMLAKA SACCOS ZANZIBAR LEO - Issa Michuzi | PressTZ - Your Number 1 Source of Aggregated Online Content

 

MAKAMU WA RAIS AZINDUA USHIRIKA WA MAMLAKA SACCOS ZANZIBAR LEO


Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan amesema Serikali zote mbili, yaani ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania inayoongozwa na Dkt. John Pombe Magufuli na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar inayoongozwa na Dkt. Ali Mohamed Shein zinaamini kuwa vyama vya Ushirika ni njia muhimu sana ya kuzalisha ajira hususan kwa wanawake na vijana.
Makamu wa Rais ameyasema hayo leo wakati wa Uzinduzi wa Ushirika wa Mamlaka Saccos uliofanyika katika ukumbi wa Abdul Wakiil, Baraza la Wawakilishi la Zamani Kikwajuni, Zanzibar.Ushirika wa Mamlaka Saccos ulianza na wanachama 55 na mpaka sasa wakati wa uzinduzi wake una wanachama 250 pamoja na mambo mengine Ushirika huo umeshatoa mikopo bila riba shilingi milioni 93 kwa wanachama 133.
Makamu wa Rais aliwapongeza wanaushirika huo kwa kusema “Ni wazo zuri sana kama mtalisimamia na kulitekeleza ipasavyo kwa haika mtajikomboa kiuchumi na kubadilisha kwa kiasi kikubwa hali zenu za maisha”Makamu wa Rais aliendelea kusema kuwa Bin... Continue reading ->


Source: Issa MichuziRead More