MAKAMU WA RAIS BENKI YA DUNIA KANDA YA AFRIKA AVUTIWA NA MAFANIKIO YA SERIKALI KATIKA KUPAMBANA NA UMASKINI KUPITIA TASAF. - Issa Michuzi | PressTZ - Your Number 1 Source of Aggregated Online Content

 

MAKAMU WA RAIS BENKI YA DUNIA KANDA YA AFRIKA AVUTIWA NA MAFANIKIO YA SERIKALI KATIKA KUPAMBANA NA UMASKINI KUPITIA TASAF.


NA Estom Sanga- DSM

Makamu wa Rais wa Benki ya Dunia Kanda ya Afrika,Dr. Hafez Ghanem amefanya ziara katika mtaa wa Mamboleo,halmashauri ya wilaya ya Temeke jijini DSM na kukutana na Walengwa wa Mpango wa Kunusuru Kaya Maskini unaotekelezwa na Serikali kupitia Mfuko wa Maendeleo ya Jamii-TASAF.

Akizungumza na Walengwa hao baada ya kukagua bidhaa wanazozitengeneza kama njia mojawapo ya kukuza kipato chao, Dr. Ghanem amesema jitihada waliyonyesha Walengwa hao ya kuuchukia Umaskini ,itaendelea kuungawa mkono na Benki hiyo ya Dunia ambayo amesema ni rafiki mkubwa wa Serikali ya Tanzania.

Dr.Ghanem ametoa rai maalum kwa Walengwa hao wa TASAF kutumia fursa hiyo kuongeza uzalishaji mali na kutumia mazingira mazuri ya kujiletea maendeleo kwani amesema ni dhahiri kuwa serikali ya Tanzania inawajali na imeonyesha utayari wa kuboresha maisha ya wananchi. Aidha Makamu huyo wa Rais wa Benki ya Dunia Kanda ya Afrika ambaye aliambatana na Mkurugenzi Mkazi wa Benki hiyo Bi. Bella Bird, a... Continue reading ->Source: Issa MichuziRead More