MAKAMU WA RAIS MGENI RASMI KONGAMANO LA BIASHARA NA UWEKEZAJI KATI YA TANZANIA NA MALAWI - Issa Michuzi | PressTZ - Your Number 1 Source of Aggregated Online Content

 

MAKAMU WA RAIS MGENI RASMI KONGAMANO LA BIASHARA NA UWEKEZAJI KATI YA TANZANIA NA MALAWI

Na Said Mwishehe, Globu ya jamiiMAKAMU wa Rais Samia Suluhu Hassan anatarajiwa kuwa mgeni rasmi katika ufunguzi wa Kongamano la Biashara kati ya Tanzania na Malawi ambalo litafanyika Julai 26 hadi Julai 27 mwaka huu mkoani Mbeya.
Kongamano hilo limeandaliwa na Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Mbeya kwa kushirikiana na Kituo cha Uwekezaji  Tanzania(TIC), Mamlaka ya Maendeleo ya Biashara Tanzania(TanTrade) pamoja na Taasisi ya Biashara na Uwekezaji ya Malawi(MITC).
Akizungumza leo jijini Dar es Salaam katika ofisi za TIC, Mkuu wa Mkoa wa Mbeya Amos Makalla amesema kauli mbiu ya kongamano hilo ni "Kuimarisha Uhusiano wa biashara na uwekezaji kati ya Tanzania na Malawi" huku lengo la kongamano hilo likiwa kuwatanisha wafanyabiashara /wawekezaji  wa nchi hizo mbili ili kubaini fursa mbalimbali za kibiashara na uwekezaji.
Ambapo amefafanua zitawezesha kuanzisha na kuendeleza miradi katika sekta za viwanda ,usafirishaji,utalii, uvuvi, kilimo ,madini, elimu, afya, benki, mawasiliano, tehama na biashara kw... Continue reading ->


Source: Issa MichuziRead More