MAKAMU WA RAIS MHE. SAMIA SULUHU HASSAN AWASILI NAMIBIA KUMWAKILISHA RAIS DKT. JOHN POMBE MAGUFULI KATIKA MKUTANO WA 38 WA SADC. - Issa Michuzi | PressTZ - Your Number 1 Source of Aggregated Online Content

 

MAKAMU WA RAIS MHE. SAMIA SULUHU HASSAN AWASILI NAMIBIA KUMWAKILISHA RAIS DKT. JOHN POMBE MAGUFULI KATIKA MKUTANO WA 38 WA SADC.

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan amewasili  Mjini Windhoek Namibia leo Agosti 15, 2018 kumuwakilisha Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli katika Mkutano wa 38 wa Wakuu wa Nchi na Serikali wa Jumuiya ya Maendeleo ya Kusini mwa Afrika (SADC), utakaofanyika tarehe 17 – 18 Agosti 2018. Katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Hosea Kutako mjini Windhoek Namibia, Makamu wa Rais amepokelewa na  Waziri wa Elimu ya Juu , Mafunzo na Ubunifu wa Namibia Mhe. Dkt. Itah Kandjii – Murangi , Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa Mhe. Christin Hoebes na viongozi mbalimbali wa Serikali ya Namibia. Hii ni sehemu ya mikutano ya awali ya maandalizi ya mkutano wa 18 wa Wakuu wa Nchi na Serikali wa SADC utakaofanyika tarehe 17 na 18 Agosti 2018 mjini Windhoek, Namibia.  Mikutano mingine ya awali ni pamoja na mkutano wa Makatibu Wakuu wa SADC uliofanyika tarehe 9 na 11 Agosti 2018 na Mkutano wa Wakuu wa Nchi na... Continue reading ->


Source: Issa MichuziRead More