Makamu wa Rais Samia Suluhu Hassan amewataka Wakazi wa mkoa wa Kigoma kupima afya zao - Issa Michuzi | PressTZ - Your Number 1 Source of Aggregated Online Content

 

Makamu wa Rais Samia Suluhu Hassan amewataka Wakazi wa mkoa wa Kigoma kupima afya zao

MAKAMU wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan amewataka Wakazi wa mkoa wa Kigoma kupima afya zao kwani kufanya hivyo kutawasaidia kujitambua na pia kutaisaidia Serikali kuwa na takwimu kamili za afya na kurahisisha utoaji huduma kwa waathirika.
Makamu wa Rais ameyasema hayo wakati wa mkutano wa hadhara uliofanyika kwenye uwanja wa mikutano wa Kazuramimba, wilaya ya Uvinza mkoani Kigoma ikiwa siku ya tatu ya ziara yake ya kukagua na kuhamasisha shughuli za kimaendeleo.
Pia alihimiza wakina mama kuzingatia lishe bora kwa watoto kuepuka athari za udumavu “Mkoa wa Kigoma unaongoza kwa uzalishaji chakula ni mkoa ambao hautuumizi kichwa katika kutafuta chakula cha Watanzania, unajitosheleza kabisa lakini kuna tatizo la lishe duni hasa kwa watoto”alisema Makamu wa Rais.
Takwimu zinaonyesha mpaka mwaka 2015 kiwango cha udumavu katika mkoa wa Kigoma ni asilimia 37.9
Makamu wa Rais amewaambia wakazi wa Kigoma kuwa na utaratibu wa kutoa taarifa hasa kwa wageni wanaoto... Continue reading ->Source: Issa MichuziRead More