Makatibu Wakuu, MaRas Watakiwa Kuzingatia Taratibu, Kanuni na Sheria kwa Maendeleo Wananchi. - Issa Michuzi | PressTZ - Your Number 1 Source of Aggregated Online Content

 

Makatibu Wakuu, MaRas Watakiwa Kuzingatia Taratibu, Kanuni na Sheria kwa Maendeleo Wananchi.

Na Frank Mvungi- MAELEZOKatibu  Mkuu Kiongozi Mhandisi Balozi John Kijazi amewataka Makatibu Wakuu wa Wizara na Makatibu Tawala wa Mikoa kutekeleza majukumu yao kwa kuzingatia Sheria , Kanuni, Taratibu na Miongozo inayotolewa na Serikali ya Awamu ya Tano  kila wanapofanya maamuzi.Akizungumza leo Jijini Dodoma wakati akifungua kikao kazi cha siku tatu kwa Viongozi hao Balozi Kijazi amesema kuwa  wanalo jukumu kubwa la kuhakikisha kuwa wanazingatia taratibu zote ili azma ya kujenga uchumi wa viwanda ifikiwe kwa wakati na kuwanufaisha wananchi.“Nafasi zenu ni za maamuzi hivyo msipofanya maamuzi sahihi na kwa wakati mtakwamisha shughuli za maendeleo na huduma muhimu kwa wananchi.” Alisisitiza Mhandisi Kijazi.Akifafanua, Mhandisi Kijazi amesema kuwa wajumbe wa mkutano huo wanalojukumu kubwa la kuhakikisha kuwa wanafanyia kazi masuala yote yatakayoazimiwa katika kikao kazi hicho cha siku tatu kinacholenga kuongeza tija katika ngazi ya Wizara na Mikoa kwa kuzingatia azma... Continue reading ->


Source: Issa MichuziRead More