Makipa hawa wamevunja benki - Shaffih Dauda | PressTZ - Your Number 1 Source of Aggregated Online Content

 

Makipa hawa wamevunja benki


Chelsea imekalisha usajili wa golikipa wa Athletic Bilbao Kepa Arrizabalaga kwa ada ya £71 milioni dau kubwa zaidi katika historia ya soka kwa upande wa makipa. Kuna wadau wanauliza imekuwaje Chelsea kutoa dau kubwa kiasi hicho. Bila shaka hawakuwa na namna kwa sabab tayati Thibaut Courtois amekimbilia Real Madrid. Je wangebaki na nani golini? Cabalero? Thubutu…!Inasemekana kuwa klabu ya Real Madrid itailipa Chelsea £35 milioni (€38.8m, $45m) pamoja na mkopo wa Mateo Kovacic. Courtois alijiunga Chelsea tokea mwaka 2011, alipotokea Genk. Alipelekwa Atletico Madrid, kwa mkopo mpaka 2014. Sakata lake la uhamisho lilianza baada ya yeye kugoma kujiunga Chelsea kwenye uwanja wao wa mazoezi wa CobhamHapa tunaangalia takwimu za usajili wa ghali wa hapo awali wa walinda lango kabla ya Keppa.


Alisson Becker, Roma kwenda Liverpool 2018, £65million

Allison Becker amejiunga na Liverpool msimu huu baada ya Karius kufanya madudu ... Continue reading ->


Source: Shaffih DaudaRead More