MAKUMBUSHO YA NYERERE KUFANYIWA DUA BAGAMOYO - Issa Michuzi | PressTZ - Your Number 1 Source of Aggregated Online Content

 

MAKUMBUSHO YA NYERERE KUFANYIWA DUA BAGAMOYO

FAMILIA ya sheikh Mohammed Ramiya, imeiangukia serikali na wizara ya utalii kuangalia uwezekano wa kuweka sehemu ya kumbukumbu kati ya hayati sheikh Ramiya na Mwl.J.K Nyerere, eneo la Zawiyani kata ya Dunda,Bagamoyo ili kuenzi historia ya ukombozi wa nchi yetu .
Aidha familia hiyo inakumbuka wakati marehemu sheikh Ramiya (78) akiugua kabla ya kufikwa na umauti wake mwaka 1985 ,Mwl. Nyerere alimchukua kumuuguza nyumbani kwake Msasani jijini Dar es salaam .
Akizungumzia namna anavyomkumbuka hayati Mwl.Nyerere, wilayani Bagamoyo mkoani Pwani, mtoto wa mwisho wa sheikh Ramiya, aitwae Ramiya Mohammed Ramiya alisema ,watalii wengi wakienda kwenye makumbusho za Bagamoyo wanakuta historia ya sheikh huyo na hayati Mwl. J.K Nyerere .
Alieleza watalii hao, huwa na shauku ya kwenda kujua historia ya picha na nyumba aliyokuwa akienda kufanyiwa dua muasisi huyo ,kisha kubarikiwa kwenda kuikomboa nchi mwaka 1961.
Ramiya alisema ,enzi hizo mwalimu Nyerere alikuwa rafiki wa sheikh Ramiya ,na alipelekwa huk... Continue reading ->


Source: Issa MichuziRead More