MAKUMBUSHO YA TAIFA YAJIPANGA KUTUMIA MITANDAO KUITANGAZA - Issa Michuzi | PressTZ - Your Number 1 Source of Aggregated Online Content

 

MAKUMBUSHO YA TAIFA YAJIPANGA KUTUMIA MITANDAO KUITANGAZA


KAIMU Mkurugenzi mkuu wa Kijiji cha Makumbusho ya Taifa Agnes Robart amesema ili kuendena na mabadiliko ya teknolojia wao kama Makumbusho ya Taifa wamejipanga kikamilifu kutumia mitandao mbalimbali ili kuendelea kuitangaza Makumbusho hiyo. 
Amesema wamejipanga vizuri huku akiwataka wazazi kuhamasika kutembelea Makumbusho kwa lengo la kuendelea kurithi tamaduni mbalimbali hususani za kale. 
Agnes ameyasema hayo leo hii jijini Dar es Salaam mbele ya waandishi wa habari katika kilele cha siku ya Makumbusho Duniani ambapo amesema lazima tuendelee kuenzi tamaduni za asili nchini. 
" Hii Makumbusho inaazimishwa kila ifikapo Mei 18 kila mwaka na lengo nikujifunza Mila na desturi ambazo wazee wetu wametuachia "amesema Agnes 
Akizungumzia Makumbusho ya Taifa amesema Makumbusho hiyo imeandaa tamasha la mama na mwana ambalo linalenga wazazi na watoto kujifunza juu ya kurithi wao. 
Pia katika kauli mbiu ya mwaka huu ni Makumbusho ni" kitovu cha utamaduni :Hatma ya mila na Desturi " na katika ji... Continue reading ->


Source: Issa MichuziRead More