MALINDI YAICHOMOLEA YANGA SC DAKIKA YA MWISHO ZANZIBAR, SARE 1-1 AMAAN - Bin Zubery | PressTZ - Your Number 1 Source of Aggregated Online Content

 

MALINDI YAICHOMOLEA YANGA SC DAKIKA YA MWISHO ZANZIBAR, SARE 1-1 AMAAN

Na Asha Kigundula, ZANZIBAR
TIMU Yanga SC imelazimishwa sare ya kufungana bao 1-1 na Malindi SC katika mchezo wa kirafiki usiku wa leo Uwanja wa Amaan, Zanzibar.
Winga Deus Kaseke alitangulia kuifungia Yanga SC bao dakika ya 16 kabla ya kiungo mshambuliaji Mohammed Ahmed Adam kuisawazishia Malindi SC dakika ya 90.
Ushindi huo unakuja siku moja baada ya Yanga kushinda 4-1 dhidi ya Mlandege SC usiku wa jana katika mechi nyingine ya kujipima nguvu kujiandaa na msimu mpya.
Mabao ya Yanga SC jana yalifungwa na nyota wa kigeni, Mnyarwanda Patrick Sibomana dakika ya 26, Mganda Juma Balinya dakika ya 36, Mnamibia Sadney Urikhob dakika ya 42 na mzalendo Mrisho Ngassa dakika ya 65.

Bao pekee na la kufutia machozi la Mlandege SC lilifungwa na Hassan Ramadhani dakika ya 88 na Yanga SC itaondoka kesho kurejea Dar es Salaam, tayari kwa mchezo wake wa kwanza wa Ligi ya Mabingwa Afrika dhidi ya Township Rollers ya Botswana Jumamosi Uwanja wa Taifa.
Katika mechi zake za awali za kujiandaa na msimu mpya, Yang... Continue reading ->Source: Bin ZuberyRead More