MALINZI AJITETEA, ADAI HANA UHAKIKA NA KIASI ANACHOIDAI TFF - Issa Michuzi | PressTZ - Your Number 1 Source of Aggregated Online Content

 

MALINZI AJITETEA, ADAI HANA UHAKIKA NA KIASI ANACHOIDAI TFF

RAIS wa zamani wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF), Jamal Malinzi ameieleza Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu kuwa hana uhakika na kiasi cha fedha anachoidai hakika lakini anaimani kuwa anaidai kwani hata siku chache kabla ya kukamatwa kwake aliikopesha TFF Sh. Milioni 15.
Amedai, alikuwa akiikopesha TFF fedha mara kwa mara kwani wakati anaingia madarakani, shirikisho hilo lilikuwa na hali ngumu kiuchumi iliyosababisha madeni makubwa kutoka Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) na kusababisha akaunti za shirikisho hilo kufungwa mara kwa mara.
Malinzi amedai hayo leo Agosti 13, 2019 wakati akitoa utetezi wake mbele ya Hakimu Mkazi Maira Kasonde, dhidi ya kesi inayomkabili ya mashtaka ya kujipatia fedha kwa njia ya udanganyifu na utakatishaji fedha baada ya kukutwa na kesi ya Kujibu.
Akiongozwa na Wakili wa utetezi Richard Rweyongeza amedai, alikuwa akiikopesha TFF fedha zake binafsi na alikuwa akifanya hivyo kupitia akaunti waliyoifungua kati yake na shirikisho hilo.
Amedai kiasi hicho... Continue reading ->
Source: Issa MichuziRead More