MAMA ASAHAU KICHANGA CHAKE UWANJA WA NDEGE, AKIKUMBUKA AKIWA HEWANI, RUBANI AGEUZA KUKIRUDIA - Issa Michuzi | PressTZ - Your Number 1 Source of Aggregated Online Content

 

MAMA ASAHAU KICHANGA CHAKE UWANJA WA NDEGE, AKIKUMBUKA AKIWA HEWANI, RUBANI AGEUZA KUKIRUDIA

Na Sultani KipingoAghalabu ndege inapopata dharura angani, waongoza ndege waliopo ardhini hawasiti kuiruhusu kurudi uwanjani, wakati mwingine kutokana na kusahaulika kitu. Majuzi kati katika uwanja wa Mflamu Abdulazizi wa Saudi Arabia mama mmoja alisahau motto wake mchanga hapo uwanjani.


Yaani huyo mama, aliyekuwa anasafiri na ndege ya Shirika la Ndege la Saudi Arabia, alisahau kichanga chake kwenye eneo la kusubiria la wanaoondoka. Kwa mujibu wa gazeti la Gulf News, japokuwa yeye ni mzazi, mama huyo alipanda hiyo ndege akiwa hana shaka na jambo lolote.


Ni wakati ndege ikiwa imeshapaa angani ndipo akakumbuka kwamba kaacha kichanga uwanjani! Na mara tu baada ya kugundua hilo, akawaarifu wahudumu wa ndege kwamba kasahau motto mchanga uwanjani, na kumfanya rubani wa Ndege namba SV832 kutoka mji mkuu wa Saudi Arabi, Jeddah, ikielekea Kuala Lumpur, Malaysia, irudi uwanjani.


Tukio hilo lilishangaza kila mtu wakiwemo wahudumu wa ndege, abiria wenzake na hata waongoza ndege uwanjani Jeddah. Video... Continue reading ->


Source: Issa MichuziRead More