Mama Kanumba Amuomba Msamaha Muna Baada Ya Kuchekelea Kifo Cha Mwanaye - Ghafla TZ | PressTZ - Your Number 1 Source of Aggregated Online Content

 

Mama Kanumba Amuomba Msamaha Muna Baada Ya Kuchekelea Kifo Cha Mwanaye

Mama mzazi wa aliyekuwa staa wa Bongo movie Steven Kanumba, Florah Mtegoa maarufu kama Mama Kanumba amefunguka na kumuangukia Muna kwa magoti baada ya Kauli yake ya kuchekelea Kifo Cha Mtoto wake Patrick.


Jambo hilo lilitokea siku chache baada ya Muna Love kufiwa  na mtoto wake Patrick wiki chache zilizopita ambapo Mama Kanumba aliibuka na kuongea Kauli hii “Muna alinitukana sana, na mungu ametenda”.


Kwenye mahojiano  na Times Fm wiki hii, Mama Kanumba alisema kwamba watu hawakumuelewa alichokimaanisha na watu walikata video fupu tu ya yale yaliyosambazwa.Muna mwanangu pole sana, ni donda hilo ambalo haliponi ni donda ndugu ila naomba unisamehe.


Sikuwa na  nia mbaya na sikuomba kitokee kilichotokea, watu walininukuu vibaya. Na wewe maneno uliyonisema mwanzoni hukujua kesho mwanangu, wote ni mapenzi ya mungu mimi sina nia mbaya”.Mama Kanumba ameomba msamaha baada ya watu kumjia juu baada ya kutoa Kauli hiyo.


The post Mama Kanumba Amuomba Msamaha Muna Baada Ya Kuchekelea Ki... Continue reading ->


Source: Ghafla TZRead More