Mama Yangu Hataki Kabisa Niimbe- Nay Wa Mitego - Ghafla TZ | PressTZ - Your Number 1 Source of Aggregated Online Content

 

Mama Yangu Hataki Kabisa Niimbe- Nay Wa Mitego

Msanii wa muziki wa Bongo fleva Emanuel Elibariki maarufu kama Nay wa Mitego ameibuka na kuweka wazi kuwa Mama yake mzazi hataki kabisa aimbe kutokana na changamoto alizowahi kumbana nazo.


Nay wa Mitego ambaye anafanya vizuri na ngoma yake ya ‘Alisema’ amewafungukia Global Publishers kuwa mama yake mzazi amemtaka kuachana na muziki na kuangalia biashara nyingine.Mama yangu hataki nifanye muziki na niendelee kuimba kwa sababu ya matatizo ninayokutana nayo katika kazi zangu kwa sababu mara ya mwisho nilipokamatwa baada ya kutoa Wimbo wa Wapo ndiyo alinikataza, aliniambia niachane na muziki nifanye shughuli nyingine maana nitakuja kufa siku si zangu.


Huu wimbo nimefanya kwa ajili ya wananchi wa Tanzania na mashabiki wa muziki wangu, nimefanya kwa ajili ya hali iliyopo kwa sasa, ninampenda sana mama yangu na huwa ninamsikiliza sana, lakini kwa Wimbo wa Alisema nilijua tu unaweza kuzua balaa (utata), lakini nilipokuwa nikiendelea na kukumbuka kauli ya mama wakati nimeingia studio na ... Continue reading ->


Source: Ghafla TZRead More