Mambo ya kutarajia katika sekta ya biashara za mtandaoni 2019 - Issa Michuzi | PressTZ - Your Number 1 Source of Aggregated Online Content

 

Mambo ya kutarajia katika sekta ya biashara za mtandaoni 2019

Kwa mujibu wa mtandao wa Statista, mpaka kufikia mwaka 2021 mauzo yatakayotokana na biashara za mtandaoni yatafikia Dola za Kimarekani trilioni 4.88. Kiasi hiko kitakuwa ni maradufu ya sasa ambapo mauzo yaliyopatikana kwa mwaka 2018 ni Dola za Kimarekani trilioni 2.84. 
Hii inaasharia kukua kwa sekta hii pamoja na kutengeneza faida kubwa kwa wauzaji wa bidhaa mbalimbali kwa njia ya mtandao duniani. 
Kasi ya ukuaji wa biashara za mtandaoni inaenda sanjari na maendeleo ya sayansi na teknolojia yanayopelekea tabia za wateja kubadilika kwa kasi. Wateja wa sasa wamekuwa na tabia tofauti ukilinganisha na awali ambapo hakukuwepo na matumizi ya mifumo ya kidigitali.
Mifumo ya kidigitali imebadili kwa kiasi kikubwa tabia za wateja ambapo watoa huduma hawana budi kubadilika ili kuendana nao. Kwa mfano, sasa hivi mtu anaweza kufanya shughuli tofauti akiwa eneo moja. Malipo ya huduma mbalimbali kwa kutumia simu ya mkononi kama vile ada, umeme, visimbuzi, maji, faini, benki, leseni na mengineyo yana... Continue reading ->


Source: Issa MichuziRead More