MAMLAKA YA CHAKULA NA DAWA (TFDA) YAFUNGUA UKURASA MPYA KWA WADAU KATIKA KUANZISHA VIWANDA VYA USINDIKAJI VYAKULA NCHINI - Issa Michuzi | PressTZ - Your Number 1 Source of Aggregated Online Content

 

MAMLAKA YA CHAKULA NA DAWA (TFDA) YAFUNGUA UKURASA MPYA KWA WADAU KATIKA KUANZISHA VIWANDA VYA USINDIKAJI VYAKULA NCHINI

 Wadau kutoka Umoja wa Miradi kwa Viziwi, wanaongalia kamera msitari wa mbele kulia, Fatina Huseni (wa kwanza), Tungi Kenneth (wa pili) wakimwangalia mkalimani wao Bi. Edna, wakati wakifuatilia mada zilizokuwa zinatolewa na TFDA. Kaimu Mkurugenzi wa Usalama wa Chakula wa TFDA, Dkt. Candida Shirima, ambaye pia alimwakilisha Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Chakula na Dawa (katikati), Meneja wa TFDA Kanda ya Mashariki, Bw. Emmanel Alphonce (kushoto) na Kaimu Meneja wa Ukaguzi wa Chakula, TFDA Makao Makuu, Bw. Lazaro Mwambole (kulia) wakifuatilia majadiliano ya wadau wenye nia ya kuanzisha viwanda vya usindikaji chakula nchini (hawapo nchini).. Picha ya pamoja baina ya viongozi wa TFDA na baadhi ya watumishi wa TFDA walioshiriki Ktika kikao hicho.  Waliokaa kutoka kushoto ni Kaimu Mkurugenzi wa Usalama wa Chakula wa TFDA, Dkt. Candida Shirima, ambaye pia alimwakilisha Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa TFDA (wa pili), Meneja wa TFDA Kanda ya Mashariki, Bw. Emmanel Alphonce (wa kwanza), Mwenyekiti mteule wa kikao hicho, Bw. Hussein Tarimo (wa tatu) na Meneja Ukaguzi wa Chakula, TFDA Makao Makuu, Bw. Lazaro Mwambole.Meneja wa TFDA Kanda ya Mashariki, Bw. Emmanel Alphonce, akisisitiza jambo kwa washiriki.
Na James Ndege – Dar es SalaamWahenga walinena “Penye Nia Pana Njia”, leo hii, usemi huu umedhihirika kuwa kweli baada ya TFDA kufanya kikao na wadau takribani 80 kutoka mikoa mbalimbali nchini, wenye nia ya kuanzisha viwanda vya usindikaji vyakula lakini pia wale wenye nia ya kuviboresha vilivyopo. Kikao kazi hiki cha siku moja kilifanyika katika Ukumbi wa Mikutano wa Margareth Ndomondo-Sigonda uliopo Makao Makuu ya TFDA, jijini Dar es Salaam tarehe 07/8/2018.
Katika hotuba ya ufunguzi wa tukio hili, Kaimu Mkurugenzi wa Usalama wa Chakula wa TFDA, Dkt. Candida Shirima, ambaye pia alimwakilisha Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Chakula na Dawa alisema, “Serikali ya Awamu ya Tano inayoongozwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli imeelekeza Taasisi za Serikali kuwezesha uanzishaji wa viwanda vingi nchini kwa kadri iwezekanavyo ili kuinua uchumi wa jamii na Taifa na haya ni matokeo ya utekelezaji wa maelekezo hayo ambapo tarehe 30 Julai, 2018, Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia Wazee na Watoto, Mhe. Ummy Mwalimu katika kikao kama hiki kilichofanyikia katika Ukumbi wa Kimataifa wa Julius Nyerere (JNICC) alielekeza TFDA kuweka mazingira rafiki ya uanzishaji wa viwanda husika nchini mara moja”.
Pamoja na mambo mengine, TFDA iliwasilisha mada zinazohusu “Mahitaji Muhimu ya Kuzingatia Katika Kuanzisha Kiwanda cha Chakula na Utaratibu wa Usajili wa Majengo na Bidhaa ambapo wadau walipata fursa ya kuuliza maswali na kupata ufafanuzi kutoka kwa wataalam wa Mamlaka hali ambayo iliwafanya wadau hao kuondoa mashaka waliyokuwa nayo kuhusu changamoto walizofikiria kwamba zingeweza kuwa kikwazo katika safari ya uanzishaji na ukuzaji viwanda vya chakula nchini.
Baada ya majadiliano ya kina, kikao kiliweka maazimio ili kurahisisha uanzishaji wa viwanda kusudiwa  ambapo Meneja wa TFDA Kanda ya Mashariki, Bw. Emmanuel Alphonce aliaahidi kwamba kuanzia tarehe 09/8/2018, atateua Afisa wake mmoja ambaye atafanya kazi maalum ya kusikiliza changamoto za wadau hao na kutoa ushauri wa namna ya kuzitatua na pia kutoa namba zake za simu sanjari na za Makao Makuu kwa mtu yeyote atakayehitaji msaada zaidi ili azma ya uanzishaji viwanda vya usindikaji vyakula itimie.


Source: Issa MichuziRead More