MAMLAKA YA HALI YA HEWA YAAMUA KUTAJA SABABU ZA KUONGEZEKA KWA JOTO NCHINI - Issa Michuzi | PressTZ - Your Number 1 Source of Aggregated Online Content

 

MAMLAKA YA HALI YA HEWA YAAMUA KUTAJA SABABU ZA KUONGEZEKA KWA JOTO NCHINI

Na Said Mwishehe,Globu ya jamii
MAMLAKA ya Hali ya Hewa Tanzania(TMA) imeamua kutoa ufafanuzi kwa jamii ya Watanzania kuhusu hali ya ongezekeo la joto katika baadhi ya maeneo hapa nchini huku ikifafanua kwenye baadhi ya mikoa joto limefikia asilimia 34.
Taarifa ya TMA kwa vyombo vya habari ambayo imetoa leo jijini Dar es Salaam imesema kwa kawaida kipindi cha Oktoba hadi Machi kila mwaka jua la utosi linakuwa katika maeneo ya kizio cha kusini mwa dunia na Tanzania ikiwa ni moja ya nchi zilizopo katika kizio cha kusini, huwa na hali ya joto kali katika maeneo mengi ikilinganishwa na miezi mingine. 
"Hapa nchini, vipindi vya jua la utosi vinafikia kilele kati ya mwishoni mwa Novemba na Desemba wakati jua la utosi likiwa linaelekea kusini (Tropiki ya Kaprikoni) na hali hiyo hujirudia tena Februari wakati jua la utosi likiwa linaelekea kaskazini (Tropiki ya Kansa). Jua la utosi huambatana na hali ya Joto kali kwa sababu kipindi hicho ndipo uso wa dunia katika eneo tajwa huwa karibu z... Continue reading ->


Source: Issa MichuziRead More