MAMLAKA ZA MAJI ZIIGE MFANO WA DAWASA KUWAUNGANISHIA MAJI WANANCHI KWA MKOPO- NAIBU WAZIRI AWESO - Issa Michuzi | PressTZ - Your Number 1 Source of Aggregated Online Content

 

MAMLAKA ZA MAJI ZIIGE MFANO WA DAWASA KUWAUNGANISHIA MAJI WANANCHI KWA MKOPO- NAIBU WAZIRI AWESO

Na Zainab Nyamka, Globu ya Jamii
NAIBU Waziri wa Maji Juma Aweso amezitaka Mamlaka za maji nchini kuiga mfano wa DAWASA wa kuwaunganishia maji wananchi kwa mkopo na kuwakata kidogo kidogo kil mwisho wa mwezi.
Aweso ameyasema hayo leo Jijini Dar es Salaam kwenye banda la maonesho la Mamlaka hiyo kupata maelezo mbalimbali kwenye Wiki ya Maji duniani iliyofikia kilele.
Akizungumza baada ya kumaliza kupata maelezo kuhusu huduma wanazozitoa kwenye banda la Mamlaka ya Majisafi na Majitaka DAWASA , Naibu Waziri amesema kuwa maji yapo ila changamoto kubwa ni wananchi wanatakiwa kuunganishwa huduma ya maji na kikubwa DAWASA waliona umuhimu na kuwaunganishia maji wananchi na kuwakata kidogo kidogo kila mwisho mwezi.
Aweso amesema, katika wiki hii ya maji watendaji wanatakiwa wajitafakari kuanzia kwenye utendaji, changamoto na mafanikio kwenye sekta ya maji pia tutambue maji ni uhai na uchumi na tutoke maofisini tuingie mtaani kutatua changamoto za maji.
“Mamlaka zote wanahakikishe wanawaunganishia... Continue reading ->


Source: Issa MichuziRead More