Man United yaichapa Chelsea 4-0 - Mwanaspoti | PressTZ - Your Number 1 Source of Aggregated Online Content

 

Man United yaichapa Chelsea 4-0

Manchester, England
NDANI ya dakika 15 za kwanza ilionekana kama Manchester United ya Ole Gunner Solskjaer inakwenda kupoteza mchezo wake wa kwanza wa Ligi Kuu ya England, ambapo ilizidiwa kila idara. Chelsea ikiongozwa na Pedro Rodriguez, Tammy Abrham na Emerson ilisukuma mashambulizi makali langoni mwa Man United.
Katika mashambulizi hayo ya Chelsea, mara mbili washambuliaji wake waligogesha mwamba wa goli huku mashuti mengine yakienda nje. Hata hivyo, dakika ya 18 shambulizi la Man United liliishia kuzalisha penalti baada ya beki wa Chelsea, Kort Zouma kumkwatua Marcus Rashford ndani ya eneo la hatari na mwamuzi Anthony Taylor kuamuru upigwe mkwaju wa penati.
Rashford akitumia ufundi mwingi alifunga penati hiyo na kuitanguliza Man United kwa bao 1-0 ambalo lilidumu hadi kipindi cha kwanza kinamalizika. Licha ya kwenda mapumziko ikiwa nyuma, lakini Chelsea ilimililki mchezo huo kwa muda wote wa dakika 45.
Kipindi cha pili, Man United iliingia uwanjani ikiwa na shauku ya kupata mabao ... Continue reading ->


Source: MwanaspotiRead More