Manara anashikiliwa polisi kwa tuhuma ya kusambaza habari ya kutekwa Mo Dewji - Bongo5 | PressTZ - Your Number 1 Source of Aggregated Online Content

 

Manara anashikiliwa polisi kwa tuhuma ya kusambaza habari ya kutekwa Mo Dewji

Afisa Habari wa klabu ya Simba, Haji Manara amekamatwa na polisi kutokana na tukio la kutekwa kwa mfanyabiashara Mohammed Dewji ‘Mo Dewji’.Kwa mujibu wa mtandao wa Mwananchi, Manara alikamatwa jana jioni na kuachiwa kabla ya leo asubuhi Oktoba 12, 2018 kukamatwa tena na polisi.


Akithibitisha kukamatwa kwa Manara, Kamanda wa Polisi Kanda Maalumu ya Dar es Salaam, Lazaro Mambosasa amesema Manara anashikiliwa kutokana na kusambaza taarifa za tukio hilo kwenye mitandao ya kijamii kwa madai ya kutumwa na familia, jambo ambalo si kweli.


Mpaka saa 9:55 alasiri ya leo Ijumaa Oktoba 12, 2018, Mo Dewji ametimiza saa 34 tangu alipotekwa Alhamisi asubuhi katika Hoteli ya Colosseum jijini Dar es Salaam.


Dewji ambaye miaka mitatu iliyopita jarida la Forbes lilimtaja kuwa tajiri namba moja Afrika kwa vijana walio chini ya miaka 40 alitekwa na Wazungu wawili waliomvizia alipokuwa akishuka kwenye gari lake ili aingie kwenye mazoezi kwenye gym ya Hoteli ya Colosseum.


Taarifa za kutekwa kwa mfanyab... Continue reading ->


Source: Bongo5Read More