MANCHESTER CITY YATWAA UBINGWA WA LIGI KUU YA UINGEREZA - Issa Michuzi | PressTZ - Your Number 1 Source of Aggregated Online Content

 

MANCHESTER CITY YATWAA UBINGWA WA LIGI KUU YA UINGEREZA


Klabu ya Manchester City imefanikiwa kutwaa ubingwa wa Ligi Kuu Soka nchini humo baada ya leo kuifunga klabu ya Brighton goli 4-1 na kufikisha alama 98.
-
Man City inachukua ubingwa huo huku Liverpool iliyokuwa inaipa ushindani mkubwa inamaliza nafasi ya pili baada ya leo kuifunga klabu ya Wolves goli 2-0 na kufikisha alama 97

Man City imetetea kombe hilo baada ya msimu uliopita kuwa mabingwa na hili ni kombe lao la nne ndani ya kipindi cha misimu 8 iliyopita

Nafasi ya 3 imechukuliwa na Chelsea yenye alama 72, nafasi ya 4 imechukuliwa na Tottenham yenye alama 71, Arsenal imechukua nafasi ya 5 baada ya kupata alama 70 huku Manchester United ikiwa nafasi ya 6 na alama 66

Kwa msimamo huo, vilabu vya Manchester City, Liverpool, Chelsea na Tottenham vimekata tiketi ya kushiriki michuano ya Klabu Bingwa Ulaya kwa msimu wa 2019/2020
... Continue reading ->





Source: Issa MichuziRead More