MANENO YA PELE YAMETIMIA MAPEMA KABISA, AKADEMI YA AZAM FC SASA NDIYO GHALA LA VIPAJI VYA WANASOKA TEGEMEO TANZANIA - Bin Zubery | PressTZ - Your Number 1 Source of Aggregated Online Content

 

MANENO YA PELE YAMETIMIA MAPEMA KABISA, AKADEMI YA AZAM FC SASA NDIYO GHALA LA VIPAJI VYA WANASOKA TEGEMEO TANZANIA

Na Mahmoud Zubeiry, DAR ES SALAAM
AKIWA katika viunga vya Azam Complex, Chamazi mjini Dar es Salaam Novemba 5, mwaka 2012, Mwanasoka bora wa zamani Afrika, Abedi Ayew Pele alisema; “Kama una akademi nzuri kama hii, kwa nini uchukue mchezaji kutoka Ghana, hii nchi yenu ina watu zaidi ya Milioni 40, mnaweza kutengeneza wachezaji wengi wazuri na nyinyi mkauza Ulaya,”.
Pele alisema hayo alipokuwa katika ziara ya kutembelea akademi ya Azam FC akiongozwa na aliyekuwa Rais wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), Leodegar Tenga, mchezaji mwenzake wa zamani wa kimataifa.
Pele aliisifia mno Akademi ya Azam na akasema italeta matunda makubwa katika soka ya Tanzania baadaye na akaitabiria Azam FC itakuwa klabu kubwa yenye hadhi sawa na Manchester United ya England kutokana na uwekezaji wake huo mzuri.
Nahodha wa Taifa Stars, Mbwana Samatta aliyeinua mkono akiwa na wachezaji zao la akademi ya Azam FC Gardiel Michael na Simon Msuva (kulia) na Himid Mao (kushoto) 

Akasema akademi ya Azam ni nzuri na bo... Continue reading ->
Source: Bin ZuberyRead More