MANISPAA YA ILALA MABINGWA WA JUMLA UMITASHUMTA - Issa Michuzi | PressTZ - Your Number 1 Source of Aggregated Online Content

 

MANISPAA YA ILALA MABINGWA WA JUMLA UMITASHUMTA

Na Heri Shaaban 
MANISPAA ya Ilala wameibuka mabingwa wa jumla katika michezo yote ya mashindano ya umoja wa Shule za Msingi Umitashumta Mkoa wa Dar es Salaam na nafasi ya pili Wilaya ya Kinondoni na nafasi ya tatu Temeke. 
Akizungumza  Dar es salaam jana, Ofisa Michezo mkoa wa Dar es Salaam Hadoph Ally amesema wameunda kikosi cha mkoa chenye wachezaji 120 ambao watakwenda Mwanza kushiriki ngazi ya Taifa.
"Mashindano ya umitashumta ngazi ya mkoa yalishirikisha timu za wilaya tano Ilala, Temeke, Ubungo, Kinondoni na Kigamboni  ambapo bingwa amepatikana katika mashindano hayo na tumeunda wachezaji 120 ambao wanasafiri kwenda kushiriki ngazi ya Taifa wakiambatana na viongozi wao 20 jumla  140,"amesema.
Kwa upande wake Ofisa Elimu Ilala  Elizabeth Thomas amepongeza ushindi wa jumla katika wilaya yake.Amesema Ilala ni mabingwa kwa mara ya tatu mfululizo imekuwa ikifanya vizuri Mashindano hayo na mwaka huu timu kutoka kutoka Dar es Salaam itarejea na vikombe vyote ngazi ya Taifa.
Amesema kam... Continue reading ->


Source: Issa MichuziRead More