MANONGA QUEEN'S KUINGIA KAMBINI KESHO KUJIANDAA NA LIGI DARAJA LA KWANZA KWA WANAWAKE NCHINI - Issa Michuzi | PressTZ - Your Number 1 Source of Aggregated Online Content

 

MANONGA QUEEN'S KUINGIA KAMBINI KESHO KUJIANDAA NA LIGI DARAJA LA KWANZA KWA WANAWAKE NCHINI

Na Leandra Gabriel, Blogu ya jamii
TIMU ya wanawake kutoka jimbo la Manonga Wilayani Igunga, Mkoani Tabora itaingia rasmi kambini kesho Augusti 13, 2018 kujiandaa na michezo ya kirafiki ili kujiweka sawa na michuano ya ligi daraja la kwanza Tanzania bara inayotarajiwa kuanza kutimua vumbi Septemba 6 mwaka huu.
Akizungumza na Blogu ya jamii msimamizi wa kambi hiyo Bi. Pendo Ndaki ambaye pia ni Mwalimu Mkuu wa shule ya sekondari Ziba ameeleza kuwa Manonga Queens ipo katika hali nzuri sana na wapo tayari kwa mashindano hayo.Ameeleza kuwa timu hiyo inayojiandaa na ligi daraja la kwanza nchini tayari imeanza kujifua vikali kabla michuano hiyo kuanza kwa kuanza kucheza mechi za kirafiki.
Aidha mlezi wa timu hiyo ambaye pia ni Mbunge wa jimbo la Manonga Mh. Seif Khamis Gulamali ameeleza kuwa wamejidhatiti kufuzu kati ya timu mbili zitakazopanda daraja na Ametoa gharama zote za awali kwa ajili ya kambi hiyo ya maandalizi.
Mh.Gulamali amehimiza wadau wengine kujitoa zaidi kwa timu hiyo ili iweze kung'ara kwa kutoa ushirikiano wa hali na mali.Timu 18 zimethibitisha kushiriki Ligi Daraja la Kwanza kwa Wanawake litakaloanza Septemba 6, mwaka huu.
Ligi hiyo itachezwa katika mfumo wa makundi na timu 2 zitapanda daraja wakati zitakazobaki zitasalia kwenye ligi daraja la Kwanza. 
Timu zilizothibitisha ushiriki wao ni:
1.Yanga Princes -Dar es Salaam2.TSC - Mwanza 3.Mapinduzi Princess -Tanga 4.Migoli Queens -Iringa 5.Ruangwa Queens -Lindi 6.Viva FC -Mtwara 7.Singida Warriors -Singida8.Katoro Queens -Geita 9.Victoria Queens -Kagera 10.Tanzanite FC -Arusha 11.Mapinduzi Queens -Njombe 12.Allans Queens -Dodoma 13.Manonga Queens -Tabora14.Abeehe Bha Kyela FC -Mbeya15.Kisarawe Queens -Pwani 16.Testimony -Kilimanjaro 17.Mbinga Queens -Ruvuma 18.Kizuka Sekondari -Morogoro 
Timu hizo shiriki ni kwa mujibu wa Afisa habari wa Shirikisho la mpira wa miguu nchini (TFF) Cliford Mario Ndimbo.


Source: Issa MichuziRead More