Manula awatoa wasiwasi Simba fainali ya Kombe la Sportpesa - Sports Kitaa | PressTZ - Your Number 1 Source of Aggregated Online Content

 

Manula awatoa wasiwasi Simba fainali ya Kombe la Sportpesa

GOLIKIPA namba moja wa Simba, Aishi Manula amesema licha ya kuwa na maumivu madogo kwenye goti, anaweza akacheza mchezo wa fainali ya Kombe la Sportpesa utakaofanyika kesho mjini hapa.
Manula aliumia katika mchezo dhidi ya Kariobang Shark, juzi alicheza dhidi ya Kakamega Homeboys huku akiwa na maumivu.
Akizungumza jana muda mfupi baada ya kumalizika kwa mazoezi ya jana asubuhi kwenye viwanja vya Rift Valley mjini hapa, Manula alisema anaendelea vizuri na anaamini mpaka kufika kesho hali yake itakuwa imeimarika zaidi.

>>TETESI ZA USAJILI SIMBA SC LEO JUMAMOSI JUNE 09,2018

Katika mazoezi hayo ya juzi, Manula alifanya mazoezi ya peke yake chini ya uangalizi wa daktari wa timu hiyo, Yassin Gembe kwa kukimbia taratibu halafu baadaye akaungana na wachezaji wenzake kwa dakika 10 za mwisho za mazoezi.
Dk. Gembe, alisema mchezaji huyo anaweza akacheza mchezo wa kesho bila matatizo.
... Continue reading ->
Source: Sports KitaaRead More