MAOFISA WA TBS WABAINI KASORO ZA UZALISHAJI NONDO - Issa Michuzi | PressTZ - Your Number 1 Source of Aggregated Online Content

 

MAOFISA WA TBS WABAINI KASORO ZA UZALISHAJI NONDO

Na Chalila Kibuda, Globu ya Jamii
MAOFISA wa Shirika la Viwango Tanzania (TBS) wameendesha ukaguzi wa kushtukizwa kwenye magodauni ya kuuza vifaa vya ujenzi jijini Dar es  Salaam na kubaini kuwepo kwa baadhi ya nondo zinazozalishwa na baadhi ya viwanda nchini zisizokidhi viwango vya ubora viliwekwa kwa mujibu wa sheria.
Ukaguzi huo ulifanyika mwishoni mwa wiki katika magodauni ya kuuza nondo yaliyopo Buguruni, Mbagala, Kariakoo na Kigamboni, jijini Dar es Salaam.
Akizungumza na waandishi wa habari wakati wa ukaguzi huo mwishoni mwa wiki, Ofisa Udhibiti Ubora wa TBS, Ramadhan Shija, alisema hatua hiyo unalenga kujiridhisha kama wazalishaji wa nondo viwandani wanafuata matakwa ya viwango husika pamoja na kutoa elimu kwa umma.
Shija, alisema ukaguzi wao umebaini baadhi ya nendo ni fupi kulingana na kiwango husika. "Nondo nyingine tumebaini kuwa ni fupi, kwani badala ya kuwa na urefu wa futi 38 zina urefu wa futi 37.6, hivyo kuna udanganyifu unaofanyika," alisema Shija.
Kwa upande wake Mk... Continue reading ->
Source: Issa MichuziRead More