MAONI YA MSOMAJI: UTENDAJI WA KUSUKUMWA MPAKA LINI? - Kajunason | PressTZ - Your Number 1 Source of Aggregated Online Content

 

MAONI YA MSOMAJI: UTENDAJI WA KUSUKUMWA MPAKA LINI?

Waraka wa BASHIR YAKUB.+255784482959.
Kama kuna watu wanapaswa kutumbuliwa ni hawa wanaosubiri mpaka rais aseme halafu ndio waanze kufukuzana na majukumu yao.
Ni ajabu tokea rais aseme alivyochoshwa na ajali, karibia barabara zote za mikoani kunawaka moto.
Makamanda wamechachamaa. Wanakagua magari, wanakagua leseni na kila cha usalama.
Unaweza kufikiri labda kabla rais hajasema ukaguzi huu ulikuwa unakatazwa.
Ni aina ya kasumba mbaya kabisa kwa yeyote mwenye majukumu. Hutendi wala hufanyi mpaka mkubwa achachamae !!!. Ni kati ya mambo mabaya sana.
Zama hizi hazihitaji watu wa aina hii. Kinachoshangaza hawaoni hata aibu. Wanatokea tu mbele ya media na kusema" kuanzia leo tukikumata umevunja sheria za barabarani sheria itachukua mkondo wak e..._ ." na maneno mengine yanayofanana na hayo.
Mtu anasema eti " kuanzia leo..",_ kwani kabla ya hapo ilitakiwa iweje. Ni mambo ya ajabu.
Nakumbuka swali muhimu ambalo karibia kila usaili(interview) huwa linaulizwa, " uwezo wa kujituma kufanya kazi bila uangal... Continue reading ->


Source: KajunasonRead More