MAPRO WATATU WAKATWA KIKOSI CHA MWISHO CHA AMUNIKE - Issa Michuzi | PressTZ - Your Number 1 Source of Aggregated Online Content

 

MAPRO WATATU WAKATWA KIKOSI CHA MWISHO CHA AMUNIKE

Kocha mkuu wa timu ya Taifa ya Tanzania, Emmanuel Amunike ametangaza kikosi cha mwisho cha wachezaji 23 ambao wataiwakilisha Tanzania kwenye fainali za mataifa Afrika (Afcon 2019) nchini Misri.
Kikosi hicho kimetangazwa rasmi jana na Kocha Amunike kimewaacha nyota kadhaa wanaochezw soka la kulipwa nje ya nchi.
Wachezaji walioachwa ni pamoja na Beki Abdi Banda wa Baroka FC ya Afrika Kusini, Shiza Kichuya wa ENNPI ya Misri na Shaaban Iddi Chilunda wa Tenerife ya Hispania.
Wengine ni magolikipa Suleiman Salula wa Malindi SC ya Zanzibar na Claryo Boniface wa u20, David Mwantika wa Azam, Freddy Tangalu na Miraj Athumani wa Lipuli na kinda wa Serengeti Boys (U17), Kelvin John ‘Mbappe’.
Akitangaza kikosi kamili cha mwisho cha  wachezaji 23  wa Taifa Stars kwa ajili ya AFCON, Amunike amewataja ni   makipa; Aishi Manula (Simba SC), Metacha Mnata (Mbao FC) na Aaron Kalambo (Tanzania Prisons).
Mabeki ni Hassan Kessy (Nkana FC, Zambia), Vincent Philipo (Mbao FC), Mohamed Hussein, Erasto Nyoni (... Continue reading ->


Source: Issa MichuziRead More