Mara: Mchungaji afariki dunia wakati akimwombea marehemu! - Bongo5 | PressTZ - Your Number 1 Source of Aggregated Online Content

 

Mara: Mchungaji afariki dunia wakati akimwombea marehemu!

Mchungaji wa Kanisa la Evangelist Assemblies of God Tanzania (EAGT) la Sirari, tarafa ya Inchugu wilayani Tarime mkoani Mara, Nestory Papaa amefariki dunia wakati akimwombea marehemu katika mji wa Kehancha nchini Kenya.


Taarifa za kuaminika zimesema mchungaji huyo alikwenda katika mji huo na rafiki zake ili kuhani msiba wa shemeji wa rafiki yake.


Akizungumza mwishoni mwa wiki wakati wa maziko ya mchungaji huyo, Diwani wa Kata ya Sirari ambaye pia ni Mwenyekiti wa Kijiji cha Mpakani, Nyangoko Paulo, amesema mchungaji huyo alifikwa na umauti baada ya kuanguka ghafla wakati akimuombea marehemu huyo.


Ndugu wa Mchungaji huyo aliyejitambulisha kwa jina Charles Papaa alisema kaka yake aliyekuwa Mchungaji wa Kanisa la EAGT lililopo katika mji wa Sirari na pia mfanyabiashara wa duka la kuuza vipodozi alikufa katikati ya maombezi aliyokuwa akiyafanya.


Mnamo Jumatano iliyopita, kaka na marafiki zake akiwemo Nyangoko Roman walikwenda kuhani msiba wa shemeji yake na Nyangoko huko Kehancha, Kenya.


... Continue reading ->


Source: Bongo5Read More