Marcelo akubali kulipa faini ya €753,000 - Shaffih Dauda | PressTZ - Your Number 1 Source of Aggregated Online Content

 

Marcelo akubali kulipa faini ya €753,000

Beki wa kushoto wa Real Madrid na timu ya taifa ya Brazil, Marcelo amekubali kulipa €753,000 kama faini ya ukwepaji kodi.

Marcelo amekubali kulipa kiasi hicho cha fedha baada ya ya kufanyika makubaliano na mwendesha mashtaka wa masuala ya kodi jijini Madrid.Mnamo mwaka jana beki huyo wa kushoto wa Real Madrid alishtumiwa kuwa alifanya janja janja ya kukwepa kiwembe cha kukata kodi kwenye mauzo ya matangazo ya tasiwira za picha zake.Wakala wa masuala ya ulipaji kodi nchini Hispania EFE mapema hivi jumanne walikuwa na majadiliano ya kina kuhusiana na sakata hilo. Marcelo aliburuzwa mahakamani na mawakala hao mjini Madrid na alikiri makosa hayo.

Marcelo kwakuwa tayari ni mtu mwenye hamasa kubwa ndani ya taifa la Hispania makosa yake ya kodi yamepunguzwa adhabu, hivyo atalipa faini pekee yake. Nyota wengine Cristiano Ronaldo na Lionel Messi wamewahi pia kukumbwa na kashikashi ya ukwepaji kodi. Hivi Majuzi kocha wa manchester United Jose Mourinho nae alinaswa kwenye mtego huo.


Kwinginek... Continue reading ->


Source: Shaffih DaudaRead More