Marcelo: hakuna kizuizi kwa Neymar Jr kujiunga Real Madrid - Sports Kitaa | PressTZ - Your Number 1 Source of Aggregated Online Content

 

Marcelo: hakuna kizuizi kwa Neymar Jr kujiunga Real Madrid

Mlinzi wa kushoto wa timu ya taifa ya Brazil, Marcelo amesema haoni kizuizi cha mchezaji mwenzake wa kikosi hicho, Neymar Jr kujiunga naye Real Madrid.

Wawili hao walio katika kambi ya timu ya taifa ya Brazil kwenye jiji la London Uingereza wakijiandaa na fainali za Kombe la Dunia zitakazofanyika nchini Urusi wamekuwa marafiki wa muda mrefu nje ya uwanja.

“Sidhani kama kuna kikwazo chochote, Neymar anaweza kujiunga na Madrid”

"Ninamkaribisha kwa mikono miwili ajiunge nasi na sidhani kama kutakuwa na tatizo na wachezaji wengine" Amesema Marcelo

Tetesi za Neymar Jr kujiunga na Real Madrid zimetajwa kumchukiza nahodha na mshambuliaji wa Ureno, Cristiano Ronaldo ambaye baada ya mchezo wa fainali ya Klabu Bingwa Ulaya dhidi ya Liverpool alisema angezungumzia mustakabali wake kwenye klabu hiyo.

Ronaldo na Gareth Bale wanatarajiwa kuondoka klabuni hapo ingawa uongozi wa Madrid umedai wawili hao watauzwa kwa bei stahiki.

Bale amekuwa akifukuziwa na Manchester United kwa miaka kadhaa huku Ronaldo n... Continue reading ->
Source: Sports KitaaRead More