MAREFA WA GABON KUCHEZESHA TAIFA STARS NA UGANDA KUFUZU AFCON JUMAPILI TAIFA - Bin Zubery | PressTZ - Your Number 1 Source of Aggregated Online Content

 

MAREFA WA GABON KUCHEZESHA TAIFA STARS NA UGANDA KUFUZU AFCON JUMAPILI TAIFA

Na Mwandishi Wetu, DAR ES SALAAM
MCHEZO wa mwisho wa Kundi L kufuzu Fainali za Kombe la Mataifa ya Afrika (AFCON) mwaka huu kati ya wenyeji, Tanzania na Uganda Jumapili wiki hii Uwanja wa Taifa mjini Dar es Salaam utachezeshwa na marefa kutoka nchini Gabon.
Hao ni Eric Arnaud Otogo Castane atakayepuliza kipyenga akisaidiwa na washika vibendera, Moussounda Montel na Marlaise Ditsoga Boris na mchezo utaanza Saa 1:00 usiku.
Wakati huo huo, mechi kati ya Cape Verde na Lesotho mjini Praia itachezeshwa na refa Mahamadou Keita atakayesaidiwa na washika vibendera Baba Yomboliba na Nouhoum Bamba, wote wa Mali mjini Praia.

Eric Arnaud Otogo Castane atachezeshwa mechi kati ya Tanzania na Uganda Jumapili Uwanja wa Taifa 

Tanzania inayofundishwa na kocha Mnigeria, Emmanuel Amunike inahitaji ushindi Jumapili ili kuangalia uwezekano wa kufuzu AFCON ya Juni nchini Misri iwapo Lesotho itafungwa au kutoa sare na Cape Verde.
Kikosi cha Taifa Stars kimekamilika kambini, hoteli ya Bahari Beach mjini Dar es Sal... Continue reading ->Source: Bin ZuberyRead More