Marekani: Asakwa na Polisi kwa tuhuma za wizi wa zawadi harusini, donge nono kutolewa kwa atakaye toa taarifa zake  - Bongo5 | PressTZ - Your Number 1 Source of Aggregated Online Content

 

Marekani: Asakwa na Polisi kwa tuhuma za wizi wa zawadi harusini, donge nono kutolewa kwa atakaye toa taarifa zake 

Polisi wanamsaka mwanamke ambae amepachikwa jina la “mvamizi wa harusi ” ambaye amekuwa akishutumiwa kuiba zawadi kutoka kwenye harusi kadhaa kusini mwa jimbo Texas nchini Marekani.


Mwanamke huyo anadaiwa kuiba zawadi za thamani ya maelfu ya dola na pesa kutoka kwa wanandoa wapya wanaooana


Mwanamke huyo ambaye hajatambuliwa amekuwa akishutumiwa kujitokeza kwenye harusi, bila mwaliko, walau katika harusi nne tangu mwezi Disemba.


Polisi pia wameushirikisha umma picha ya mwnamke huyo akiwa dukani akijaribu kutumia kadi ya zawadi ambayo awali ilitumiwa na wanandoa waliofanya harusi karibuni.


Zawadi ya dola 4,000 sawa na zaidi ya milioni Tisa za Kitanzania, (pauni 3,300) imetangazwa kwa mtu yeyote atakayetoa taarifa zitakazosaidia kukamatwa kwake.


“Tusiache aharibu siku maalum ya mtu yeyote na tumlete mvamizi huyu wa harusi za watu mbele ya sheria ,” imesema taarifa ya ofisi ya mkuu wa polisi wa kaunti ya Comal – Texas.


Bodi ya maandalizi ya harusi katika eneo hilo imekiambia kituo cha habari cha CBS kuwa inatambua sura za watu waliopiga picha za harusi


“Tumekuwa na harusi za wazi msi... Continue reading ->


Source: Bongo5Read More