Marekani yaijibu Iran shambulio la bomu, yaitaka ijiangalie - Bongo5 | PressTZ - Your Number 1 Source of Aggregated Online Content

 

Marekani yaijibu Iran shambulio la bomu, yaitaka ijiangalie

Balozi wa Marekani umoja wa mataifa ameitaka Iran ijiangalie yenyewe katika shambulio la la kijeshi lililoua watu 25 siku ya Jumamosi.Wanajeshi wa Iran wakionekana mtaani baada ya mtaa wa Ahvaz kushambuliwa na wanao daiwa kuwa magaidi Septemba 22 mwaka 2018 na kuripotiwa vifo vya watu 25.


Kwa mujibu wa shirika la habari la BBC balozi huyo, Nikki Haley amejibu tuhuma za rais wa Iran, anayeilaumu Marekani kwa kuhusika na shambulio hilo na kusema kuwa Marekani imewagandamiza watu wake kwa muda mrefu sasa”.


Makundi mawili yamedai kuhusika na shambulio hilo licha ya kutowasilisha ushahidi wao.


Watu wanne waliokuwa na bunduki walishambulia wanajeshi wa mapinduzi ya Iran Kusini Magharibi mwa mji wa Ahvaz siku ya jumamosi na kuua watu 25 ambao ni wanajeshi pamoja na raia akiwemo msichana mdogo wa miaka mine waliokuwa wakiangalia maadhimisho ya gwaride la kumbukumbu ya mapinduzi ya kijeshi ya Iran.


Nani wa kulaumiwa?


Makundi yanayoipinga serikali ya Iran ya Ahvaz National Resistance na Isla... Continue reading ->


Source: Bongo5Read More