Marekani yalivalia njuga suala la kupotea mwandishi Khashoggi,yaiomba Uturuki kutoa kanda za ushahidi - Bongo5 | PressTZ - Your Number 1 Source of Aggregated Online Content

 

Marekani yalivalia njuga suala la kupotea mwandishi Khashoggi,yaiomba Uturuki kutoa kanda za ushahidi

Marekani imeomba Uturuki kutoa ushahidi wa kanda ya sauti inayodai kuwa mwanahabari wa Saudi Arabia Jamal Khashoggi aliuawa ndani ya ubalozi wa Saudi Arabia mjini Istanbul. Rais Trump amewaambia waandishi katika ikulu ya White House kuwa, “Tumeomba kupewa nakala kanda hiyo, kama ni kweli ipo,”.Mtoto mdogo akishikilia picha ya mwanahabari wa Saudi Arabia Jamal Khashoggi


Bwana Khashoggi hajawahi kuonekana tangu alipoingia jengo la ubalozi wa Saudi Arabia tarehe mbili mwezi huu wa Oktoba.  Saudi Arabia amekanusha madai yakuhusika na kutoweka kwa mwandishi huyo.


Huku hayo yakijiri, Gazeti la Washington Post limechapisha makala ya mwisho yaliyoandikwa na bwana Khashoggi kabla ya kutoweka kwake. Katika makala hayo anazungumzia umuhimu wa uhuru wa vyombo vya habari katika eneo la Mashariki ya kati.


Mhariri wa kimataifa wa gazeti hilo Karen Attiah amesema uchapishaji wa makala hayo ulisitishwa kwa ajili ya kuwa na matumaini kwamba bwana Khashoggi atarejea salama. Aliandika akisema “Sa... Continue reading ->


Source: Bongo5Read More