MAREKANI YATOA VIFAA VYA KUPIMIA MAJI KWA BODI ZA MABONDE YA MAJI RUFIJI NA WAMI/RUVU - Kajunason | PressTZ - Your Number 1 Source of Aggregated Online Content

 

MAREKANI YATOA VIFAA VYA KUPIMIA MAJI KWA BODI ZA MABONDE YA MAJI RUFIJI NA WAMI/RUVU

Serikali ya Marekani ilikabidhi vifaa vya kupimia maji kwa Bodi za Mabonde ya Maji Rufiji na Wami / Ruvu. Vifaa na huduma za ziada vitasaidia bodi kukusanya na kuchambua takwimu juu ya ubora na kiasi cha maji. Ufuatiliaji wa uboreshaji wa maji utasaidia wilaya kufanya maamuzi sahihi juu ya ugawaji wa maji ili kusimamia na kulinda rasilimali za maji kwa vizazi vijavyo.
Mbali na vifaa vya kupimia maji, Bodi za Maji zilipata boti/mashua, kompyuta, redio, vifaa vya kukadiria umbali, na vifaa vya mtandao kwa shughuli za zinazofanyika katika eneo la mradi na ofisini. Wafanyakazi watafundishwa namna ya kutumia vifaa vya kupimia maji ya mtoni.
Vifaa na huduma, vyenye thamani ya shilingi bilioni 2.3 za Kitanzania (dola 980,000 za Kimarekani), zilikabidhiwa na Shirika la WARIDI, na kufadhiliwa na Shirika la Marekani la Maendeleo ya Kimataifa (USAID). WARIDI inaendeleza usimamizi wa rasilimali maji na kuboresha upatikanaji wa huduma za maji.
"Kwa sababu maji yana jukumu muhimu katika kupunguza umasiki... Continue reading ->


Source: KajunasonRead More