MASAUNI AFUNGUA SEMINA YA VIONGOZI WA TAASISI ZA KIISLAM JIJINI DAR ES SALAAM - Issa Michuzi | PressTZ - Your Number 1 Source of Aggregated Online Content

 

MASAUNI AFUNGUA SEMINA YA VIONGOZI WA TAASISI ZA KIISLAM JIJINI DAR ES SALAAM

Serikali imesema haitakua tayari kuona Amani na Utulivu wa Nchi inachezewa huku ikisisitiza uwepo wa Umoja kati ya wananchi bila kujali tofauti ya imani, kabila au itikadi yoyote.
Hayo yamesemwa na Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni wakati akifungua Semina ya siku mbili iliyofanyika jijini Dar es Salaam ikiwahusisha Viongozi wa Taasisi za Kiislamu lengo ikiwa ni kuwakumbusha kuhubiri amani katika sehemu zao
Amesema muelekeo na malengo ya Serikali ya Awamu ya Tano ni kukuza maendeleo katika sehemu mbalimbali nchini lengo ikiwa kuinua maisha ya wananchi nan chi kwa ujumla
“Serikali hii imejidhatiti kuhakikisha maendeleo yanakuja kwa kasi na maendeleo hayawezi kuja ikiwa amani na utulivu haupo, sisi kama serikali tutahakikisha tunalinda amani iliyopo ili wananchi wapate kufanya shughuli za kiuchumi bila wasiwasi wowote” alisema Masauni
Akizungumza wakati wa ufunguzi huo, Sheikh wa Mkoa wa Dar es Salaam, Alhaji Mussa Salum aliihakikishia serikali kutokuwepo ... Continue reading ->


Source: Issa MichuziRead More