Masauni aokoa Milioni Mia Mbili za Rais Magufuli - Issa Michuzi | PressTZ - Your Number 1 Source of Aggregated Online Content

 

Masauni aokoa Milioni Mia Mbili za Rais Magufuli

Jeshi la Polisi nchini limeelekezwa kutumia wafungwa ili kuweza kuokoa kiasi cha Shilingi Milioni Mia Mbili  kati ya Milioni Mia Saba zilizotolewa na Rais Dk. John Magufuli   katika Mradi wa Ujenzi wa Mabweni na Madarasa ya  Chuo cha Taaluma ya Polisi kilichopo  Kurasini jijini Dar es Salaam.
Maelekezo hayo yametolewa na Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni alipotembelea majengo chakavu ya chuo hicho baada ya kupokea kiasi cha Shilingi Milioni Mia Saba alizoahidi Rais Dkt. John Magufuli akihutubia katika mahafali ya kuhitimisha Mafunzo ya Kozi za Uofisa na Ukaguzi Msaidizi  chuoni hapo mwishoni mwa mwaka jana
“Wizara ina taasisi ya magereza ambayo ina nguvu kazi ya kutosha, na Rais alishaagiza wafungwa watumike katika shughuli za uzalishaji, sioni sababu ya kutumia kiasi hicho cha pesa kuwalipa vibarua wa nje, naagiza muwasiliane na Jeshi la Magereza pamoja na kikosi cha ufundi kilichopo ndani ya Jeshi la Polisi ili muweze kuona ni vipi mnaokoa kiasi hic... Continue reading ->


Source: Issa MichuziRead More