MASAUNI AONGOZA KIKAO CHA KWANZA CHA BARAZA JIPYA LA TAIFA LA USALAMA BARABARANI - Issa Michuzi | PressTZ - Your Number 1 Source of Aggregated Online Content

 

MASAUNI AONGOZA KIKAO CHA KWANZA CHA BARAZA JIPYA LA TAIFA LA USALAMA BARABARANI

AWATAKA WAJUMBE WALIOTEULIWA WATHIBITI AJALI NCHININaibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, ambaye pia ni Mwenyekiti wa Baraza la Taifa la Usalama Barabarani, Mhandisi Hamad Masauni, akizungumza na wajumbe wapya wa Baraza hilo ambalo lilizinduliwa hivi karibuni baada ya kuvunjwa na Waziri wa Wizara hiyo mwezi Julai mwaka huu. Kushoto meza kuu ni Naibu Waziri wa Wizara ya Ujenzi, ambaye pia ni Makamu Mwenyekiti wa Baraza hilo, Elius Kwandikwa. Kulia ni Mkuu wa Kikosi cha Usalama Barabarani ambaye pia ni Katibu wa Baraza hilo, Fortunatus Musilimu. Kikao hicho kilifanyika katika Ukumbi wa Mikutano wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, jijini Dodoma, leo. Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, ambaye pia ni Mwenyekiti wa Baraza la Taifa la Usalama Barabarani, Mhandisi Hamad Masauni (katikati), akifurahi jambo wakati Naibu Waziri wa Wizara ya Ujenzi, ambaye pia ni Makamu Mwenyekiti wa Baraza hilo, Elius Kwandikwa (kushoto) alipokua anazungumza katika kikao cha kwanza cha Baraza hilo tangu l... Continue reading ->


Source: Issa MichuziRead More