Masha amiliki asilimia 68 ya hisa kampuni ya Fastjet - Mwanaharakati Mzalendo | PressTZ - Your Number 1 Source of Aggregated Online Content

 

Masha amiliki asilimia 68 ya hisa kampuni ya Fastjet


Waziri  wa zamani wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Lawrence Masha, amenunua asilimia 64 ya hisa za kampuni ya ndege ya Fastjet Tanzania, hivyo kuongeza hisa zake kufikia asilimia 68 kutoka asilimia nne aliyokuwa akimiliki awali.
 
Ofisa Uhusiano na Masoko wa Fastjet, Lucy Mbogoro, jana alisema Masha alinunua hisa hizo ikiwa ni sehemu ya mpango wa kuimarisha na kuboresha kampuni hiyo, kuelekea katika mikakati mipya ya kuboresha huduma inayotarajiwa kuanza mwakani.

Alisema Masha ambaye kwa sasa ni Mwenyekiti Mtendaji wa Fastjet amenunua hisa hizo ambazo ni asilimia 17 zilizokuwa zikimilikiwa na Kampuni mama ya Fastjet PLC ya Afrika Kusini na asilimia 47 ya hisa zilizokuwa zikimilikiwa na wazawa, ikiwa ni hatua ya kuifanya kampuni hiyo imilikiwe moja kwa moja na Watanzania.

“Kwa sasa ieleweke kwamba asilimia 68 ya hisa zote za Fastjet nchini inamilikiwa na Lawrence Masha na thamani halisi ya hisa hizo itatajwa baadaye, baada ya kuweka mambo yote sawa. Ila hii ni sehemu ya kuifanya kampuni hii i... Continue reading ->
Source: Mwanaharakati MzalendoRead More