Mashahidi 54 na vielelezo 218 kuwasilishwa Mahakama Kuu Divisheni ya Rushwa na Uhujumu uchumi Kesi ya kina Kitillya - Issa Michuzi | PressTZ - Your Number 1 Source of Aggregated Online Content

 

Mashahidi 54 na vielelezo 218 kuwasilishwa Mahakama Kuu Divisheni ya Rushwa na Uhujumu uchumi Kesi ya kina Kitillya

Na Karama Kenyunko, Globu ya Jamii. 
JUMLA  ya Mashahidi 54 na vielelezo 218 vinatarajiwa kuwasilishwa Mahakama Kuu Divisheni ya Rushwa na Uhujumu uchumi, katika kesi ya Uhujumu uchumi inayomkabili aliyekuwa Kamishina Mkuu wa Mamlaka ya Mapato Tanzania  (TRA), Harry Kitillya na wenzake wanne kwa ajili ya kwenda kuanza kusikilizwa.
Mbali na Kitilya washtakiwa wengine katika kesi hiyo ni  Maofisa wa benki ya Stanbic, Shose Sinare na Sioi Solomon, Kamishna wa Sera ya uchambuzi wa Madeni kutoka Wizara Fedha na Mipango, Bedason Shallanda na msaidizi wake Alfred Misana ambapo wote wanakabiliwa na mashtaka 58 yakiwemo ya utakatishaji fedha.
Hatua hiyo imekuja huku tayari Kitilya na wenzake wawili Shoe na Sioi wakiwa wamekaa gerezani kwa takribani miaka mitatu ambapo walifikishwa mahakamani hapo kwa mara ya kwanza Aprili 16, 2016. Kesi hiyo imehamishiwa Katika mahakama ya mafisadi leo Februari 12, 2019 mara baada ya washtakiwa kusomewa upya mashtaka yao na kutajiwa Idadi ya mashahidi na viele... Continue reading ->


Source: Issa MichuziRead More